![]() |
Advertisement |
Protective style kwa kiswahili ni Msuko kinga, huu unasukwa ili kuzikinga nywele za asali au za dawa kukatika, kuharibika na hivyo kuzifanya zikue vizuri na zisiwe nausumbufu wowote.
π§♀️Msuko kinga au protective style ni msuko ambao unaweza kukaa kichwani kwako kuanzia siku tano na kuendelea, mpaka mwezi inatokana na aina ya nywele.
Msuko kinga (Protective style) unaweza kuwa;
π Nywele za rasta (box braids)
πNywele za mkono (flat twist)
πNywele za uzi (african threads) nk.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA YA KUSUKA
π§♀️Osha nywele zako kwa shampoo; Unashauriwa utumie sulfate free shampoo.
(Kwa nini utumie sulfate free shampoo nilifundisha, post zilizopita pitia)
π§♀️Fanya deep conditioner (steaming)
Hii huzuia nywele kukatika, inakuza nywele na kufanya nywele ziwe na afya; Utakaa na steaming ndani ya nusu saa au dakika 30.
π§♀️Detangle nywele zako ipasavyo
π§♀️Chana nywele zako kuanzia juu kushuka chini,wengi tumezoea kuchana kuaanzia chini kupanda juu lakini hii ina madhara mengi kama vile:
-Inasababisha nywele kukatika
-Nywele utaona hazikui
π§♀️Unachana nywele kimafungu kama ni ndefu na nyingi; yaani zilizojaa
π§♀️Hakikisha unatumia chanuo lenye meno mapana.
π§♀️Moisturize (zipe nywele zako unyevu.
Kwa nini tunazipa unyevu kwa sababu nywele kavu ni rahisi kukatika,huwa ngumu na kuuma pia.
π§♀️Baada ya hapo suka msuko wako.
0 comments: