![]() |
Advertisement |
NJIA YA KWANZA
π§π»♂️Chukua nazi iliyokomaa vizuri
π§π»♂️Iache mpaka iharibike
π§π»♂️Baada ya hapo toa nazi na uweke kwenye blender, food processor au kikunio ili iweze kulainika
vizuri
π§π»♂️Ongeza maji ya vuguvugu na kamua tui
π§π»♂️Chemsha tui na mchai chai pamoja mpaka uone mafuta yanabakia,
π§π»♂️Ondoa majanu ya mchai chai na kutoa mafuta yako na kuyaweka kwenye chombo chako ili utumie.
NB: Njia hii inakufanya uweze kupata mafuta mengi zaidi na pia mchai chai una manufaa sana katika kufanya mwili na ngozi (hasa ya kichwa) kurelax sasa ukichanganya wakati wa kuchemsha utaweza kupata virutubisho vyingi zaidi kwenye mafuta; ambavyo vitakua na faida kwenye nywele pamoja na ngozi.
Pia mara nyingine mafuta ya nazi huwa na harufu, usiwe na shaka hapa pia nitakupa njia ya kuondoa harufu iyo na kubaki na harufu iliyopoa.
JINSI YA KUONDOA HARUFU KWENYE MAFUTA YA NAZI
πChukua sufuria kubwa weka maji na kuyaweka kwenye moto. (medi-High temperature yaani moto wa kawaida usiwe mkali sanaa).
πChukua sufuria ndogo weka mafuta yako ya nazi.
πChukua mchai mchai (green tea. Changanya kwenye mafuta yako.).
πWeka sufuria yenye mchanganyiko wa mafuta na mchai chai juu ya safuria yenye maji na kupika kwa muda wa dakika kama 30 hivi.
πOndoa majani na weka mafuta yako kwenye chombo cha kutumia.
πMafuta yako yatakua tayari kutumia.
ITAENDELEA NIKIELEZEA NJIA YA PILI NA YA TATU
0 comments: