![]() |
| Advertisement |
MAHITAJI
๐ง๐ป♂️Chanuo kubwa
๐ง๐ป♂️Spray bottle yenye maji
๐ง๐ป♂️Mafuta ya kimiminika (Mafuta ya nazi/Olive oil/Black castor oil-au waweza changanya yote kwa viwango sawa sawa)
๐ง๐ป♂️Leave in conditioner (Ya chaguo lako-nzuri zaidi ni za Auntie Jackies au Cantu products)
๐ง๐ป♂️Applicator bottle
JINSI YA KUFANYA
๐Weka maji kwenye spray bottle
๐Ongeza leave in conditioner kidogo
๐Ongeza mafuta kidogo pia kisha tikisa vizuri mchanganyiko wako
๐Spray mchanganyiko wako katika nywele kiasi sio sana
NB: Tunaspray huo mchanganyiko kwa sababu inasaidia kuongeza unyevu (moisture) na kurahisisha kuchana kucha nywele maana haitakiwi kuchana nywele zikiwa kavu. Kwa kuwa ukichana nywele kavu ni rahisi kukatika.
๐Baada ya hapo tumia vidole vyako kukata nywele mafungu, kuanzia mafungu 4 hadi 6 kulingana na nywele zako kama ndefu au fupi
๐Chana kwa kutumia vidole huku ukichambua mpaka uone nywele zimechambuka vizuri na hazijajifunga kwa kuwa 4 type hair (ambazo waafrica wengi wanazo) asili yake kujifunga hii inaitwa finger detangle husaidia kutoa nywele zilizojifunga.
๐ Chukua kitana kikubwa,chana kuanzia juu ya nywele kuja chini taratibu
๐Then unaweza kutwist,au kusuka mabutu au tumia kibanio kubana nyweke zilizochanika vizur then unahamia fungu lingine mpaka utakapomaliza zote
Hii ina faida nyingi sana kama vile;
๐Inasaidia kutokata nywele wala kutoumia wakati wa kuchana sababu nywele zinakuwa na unyevu wa kutosha halafu zimechambuka vizuri.
Pia unashauriwa unapoweka deep conditioner (steaming kwa lugha iliyozoeleka) hakikisha umechana nywele zako vizuri ili kufanya nywele zilainike na steaming iziguse au izifikie nywele zote.




0 comments: