![]() |
Advertisement |
Mapishi haya yanaweza kupika samaki aina yeyote – mbichi, aliyekaushwa au aliyekaangwa. Ni maalumu kwa kubadilisha ladha ya mapishi kutokana na chaguo la samaki wako. Unaweza kupata njia tofauti za kuongeza ujuzi wa kuandaa samaki wako.
Mahitaji
- Samaki 2 (Tunatumia samaki wabichi)
- Vitunguu maji
- Vitunguu saumu
- Nyanya
- Mafuta
- Ndimu
- Chumvi
- Carrots
- Tangawizi
- Pilipili hoho
Maelekezo
- Andaa vitunguu saumu, tangawizi na ndimu. Tenga kitunguu saumu kwenye sehemu mbili.
- Osha na kisha marinate samaki wako – weka tangawizi, vitunguu saumu, ndimu na chumvi.
- Acha samaki akae kiasi – ikiwezekana kwenye jokofu – ili viungo viingie vizuri.
- Menya vitunguu, nyanya, pilipili hoho na karoti na kisha kata vipande vidogo.
- Weka mafuta kwenye kikaangio kilicho jikoni. Subiria yapate moto vizuri.
- Weka samaki na ukaange hadi aive vizuri. Ukimaliza weka samaki pembeni.
- Bandika sufuria, weka mafuta uliyokaangia samaki. Subiria yapate moto vizuri kisha weka vitunguu na uvikaange mpaka viwe vya kahawia.
- Weka pilipili hoho na koroga mchanganyiko.
- Weka vitunguu saumu huku ukiendelea kukoroga kuzuia visigande kwenye sufuria.
- Weka karoti na endela kukoroga
- Weka nyanya kisha funika kwa muda wa dakika 5. Hakikisha kuwa moto si mkali sana, bali uwe wa wastani.
- Kamulia ndimu kwenye mchanganyiko na weka chumvi kisha koroga kiasi.
- Weka samaki na ongeza maji kiasi (usifanye hapo kwa mama ntilie mchuzi maji tu, hapo nyumbani jaribu kuandaa mchuzi mzito)
- Acha mboga ichemeke. Maji yakikaukia mchuzi wako utakua tayari na unaweza kula na chakula chochote.
0 comments: