![]() |
Advertisement |
FAIDA ZA MAJANI YA CHAI KWENYE NYWELE
-Yanajaza nywele
-Yanang’arisha nywele
-Yanarudisha rangi ya asili ya nywele zako na kuzipendezesha zaidi
-Yanazuia nywele kukatika
-Yanarefusha nywele kama inavotakiwa
NB: Kuna njia nyingi za kutumia maji ya majani ya chai kwenye nywele
1. Unaweza kuchanganya kwenye steaming yako
2. Unaweza kusuuzia nywele zako baada ya kuosha
NJIA YA KWANZA
-Chukua vijiko vitatu vya majani ya chai weka kwenye sufuria safi
-Baada ya hapo ongeza maji nusu lita
-Acha yachemle kwa dakika 5 hadi 10 kisha yaache yapoe kabisa
-Baada ya hapo chuja upate maji ya majani ya chai bila makapi
-Baada ya kuosha nywele na shampoo na kusuuza na maji ya kawaida zimwagie nywele zako maji hayo uliyoandaa (ukimaliza hapo usioshe tena nywele)
-Unaweza endelea kupaka steaming yako uliyoiandaa
NJIA YA PILI
Mahitaji
-Vijiko vitatu (3) vya maji ya chai
-Tui la nazi
-Mafuta ya nywele (Castor oil/Coconut oil)
JINSI YA KUFANYA
-Changanya vyote kwenye bakuli moja
-Paka kwenye nywele zako vizuri
-Vaa kofia ya plastic au kaa kwenye steamer kwa dk 30 hadi 45.
-Osha nywele zako vizuri na maji ya kawaida halafu unaweza suuza tena na maji ya chai uliyokwisha andaa hapo awali.
0 comments: