![]() |
Advertisement |
Bamia zinaweza kutumika kama:
🍃Leave in conditioner
🍃Steaming
🍃Kiungo cha kuondoa mba
🍃Kulainisha ngozi ya kichwa
🍃Kufanya nywele kuwa imara na rahisi kuzitunza
🍃Unaweza kutumia kusukia au kustyle nywele zako pia
Mahitaji
🍃Bamia kumi (10)
🍃Mafuta ya maji (African Black castor oil au coconut oil au olive oil)
🍃Juice ya Tangawizi
🍃Asali
Jinsi ya kuandaa
🌿Osha bamia zako vizuri kuondoa uchafu wote
🌿unaweza kukata kata kuwa vipande vidogo vidogo au ukamenya tu (kuexpose undani wake)
🌿Weka kwenye sufuria yako safi
🌿Ongeza maji kiasi (kikombe kimoja au viwili vinatosha) na ufunike
🌿Chemsha kwa dakika 10 hadi 15 mpaka ile gelly au ute wa bamia uwe umetoka wa kutosha
🌿Epua na uache ipoe kwa dakika kadhaa
🌿Baada ya hapo chuja kuondoa vipeke na upate gelly tuu
Kama unatengeneza steaming
🌿chukua ute ulioupata gawanya mara mbili
🌿Nusu ya kwanza changanya na tangawizi na asali na mafuta yoyote ya kimiminika (hasa Castor oil)
🌿Baada ya kuosha nywele kwa shampoo (hakikisha nywele zako ni safi) paka mchanganyiko kwenye nywele zote
🌿Vaa shower cap au steamer na ukae kwa dakika 30+
🌿Osha kwa maji mengi
🌿Chukua ule mchanganyiko uliobaki changanya na mafuta kijiko kimoja hapa utakua umepata (Leave in Conditioner)
🌿Nywele zako zikiwa mbichi na safi pakaa vizuri kuanzia kwenye ngozi hadi kwenye ncha.
🌿Chambua vizuri nywele zako kidodgo kidogo kuhakikisha imeingia vizuri kwenywe nywele zote.
🌿Unaweza kusuka mabutu (bantu knots) au twists za njia mbili au tatu au nywele za mistari kawaida nywele lazima ziwe na unyevu kabisa.
🌿Ukiona zinakauka unanyunyiza maji tena.
🌿Ukimaliza acha zikauke vizuri utaendelea kupaka mafuta yako kama kawaida ili kuzifanya zing’ae.
🌿Ukifumua unapata mawimbi mazuri unaweza kubana utakavyo nywele zako.
Faida zake
🍃Jelly ya bei rahisi kwa nywele za kuvutia
🍃Hutumia muda mchache kuandaa
🍃kirutubisho muhimu kwenye nywele
🍃kung’arisha nywele zako kama ilivyo kwa Alovera
NB: kwa wale wenye dawa unaweza kutumia kama leave in conditioner.
Pia ni nzuri sana kwa nywele za watoto maana haina kemikali.
0 comments: