![]() |
| Advertisement |
π§π»♀️Husaidia nywele kuwa nyevu wakati wote pia zenye muonekano mzuri, pia zitakua laini wakati wa kuchana
π§π»♀️Parachichi kina potasium na amino acids za kutosha, hivyo husaidia kukuza nywele haraka sana
π§π»♀️Kuwa na mba sana kichwani inamaana ngozi yako ya kichwa haina mafuta yani ikavu so parachichi husaidia kuongeza mafuta kwenye ngozi yako ya kichwa.
π§π»♀️Pia parachichi husaidia kufufua na kukuza nywele zilizodhoofu na kukatika sana.
UNAWEZA KUTUMIA PARACHICHI KAMA;
π₯°DEEP CONDITIONER
Aina hii unaweza fanya kila wiki au kila baada ya wiki mbili kulingana na ratiba yako.
MAHITAJI
π§π»♀️Parachichi nusu
π§π»♀️Asali kijiko kimoja
π§π»♀️Mafuta ya castor oil/Nazi/olive oil kijiko 1
JINSI YA KUANDAA
-Andaa parachichi toa maganda
-Kata vipande vidogo kulingana na uwezo wa blender yako, kisha saga kwa blender vizuri hadi usagike vizuri.
-Weka asali, kisha weka mafuta na mask/steaming yako iko tayari
JINSI YA KUTUMIA
-Paka mchanganyiko huu kuanzia kwenye mzizi wa nywele hadi kwenye ncha ya nywele.
-Massage kuchanganya
-Vaa kofia yako ya plastic kaa dk 30 mpaka 40 kisha osha nywele yako.
π₯°PROTEIN TREATMENT
Hii unatakiwa kutumia mara1 kwa mwezi au mara1 kwa wiki 6.
MAHITAJI
π§π»♀️Parachichi nusu
π§π»♀️Kiini cha yai
π§π»♀️Asali kijiko kimoja
π§π»♀️Mtindi au mayonisse
π§π»♀️Mafuta ya castor oil/Nazi/olive oil kijiko 1
BAADA YA HAPO UNAFUATA PROCESS YA KUTENGENEZA KAMA STEAMING YA KAWAIDA.





0 comments: